NAFASI ZA MASOMO KIDATO CHA KWANZA 2024 HAGAFILO SEKONDARI NJOMBE.

Kufuatia maboresho ya mitaala ya Elimu iliyofanywa na serikali. Kwa kurejelea waraka wa Elimu namba 5 wa mwaka 2023 kuhusu utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa. Hagafilo Sekondari ni shule pekee iliyoteuliwa na serikali katika Mkoa wa NJOMBE miongoni mwa Shule  chache nchini Tanzania kufundisha ufundi wa umeme wa viwandani na nyumbani.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Hagafilo anawakaribisha Wazazi,Walezi na Wanafunzi kutumia fulsa hii muhimu na adhimu sana kwa vijana wa kike na kiume kusomea utaalamu wa umeme kuanzia kidato cha kwanza 2024.

s001

Shule ya Sekondari  Hagafilo ni Shule ya bweni kwa wasichana na wavulana, yenye walimu wa kutosha, wenye elimu na taaluma bora,weledi na ari ya kumsaidia mwanafunzi,pia ni shule yenye mazingira bora na tulivu kwa kusoma na kujifunza.

Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni Hagafilo au bofya .

Watakao wahi ndiyo watakaopata nafasi. Wahi  nafasi ni chache.

Kwa mawasiliano zaidi

Mpigie Mkuu wa Shule kwa Namba : 0758-396202.